Diamond Platnumz Atangaza Fursa Kwa Vijana Wenye Vipaji.

Msanii wa Bongo Fleva ambaye ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, Diamond Platnumz ametangaza fursa kwa vijana ambao wana vipaji vya kucheza mpira wa miguu.

Hii leo Wasafi Media imezindua Kivumbi Cup, Ligi ambayo inarajia kukutanisha idadi kubwa ya vijana.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instgram, Diamond
Platnumz ameandika ujumbe kuhusiana na Ligi huyo.

"Mwenyezi Mungu katujaalia nafasi na connection mbalimbali duniani, na tukiwa kama vijana wa kutokea mtaani, tutahakikisha tunatumia nafasi hizo kadri ya uwezo wetu kusaidia vijana wenzetu mbalimbali mtaani,"

"Leo tumezindua rasmi Kivumbi Cup mashindano ya mpira wa miguu wa mtaani kwa kuamini kuwa mtaani kuna vipaji vingi havijapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao,"

"Naamini kupitia Kivumbi Cup itafungua milango mingi ya kimataifa kwa vijana wenzetu wengi wenye vipaji vya kucheza mpira,"

"Ombi langu kwa wenye team husika na makocha “tafadhali shindano hili linatazamwa kwa umakini na watu mbalimbali duniani, tujitahidi sana kupanga wachezaji wenye vipaji vya kweli, ili dunia ipate kuona vipaji tulivyo navyo na kesho na kesho kutwa wakatuwakilishe vyema ulimwenguni”.

Maoni