Unaikumbuka Hii Filamu 'Hatya' Ya Govinda

KUNA UZURI NDANI YA WANAOITWA WABAYA
KUNA UBAYA NDANI YA WANAOITWA WAZURI

Pamoja na ubaya alionayo Govinda kwa kuwa mlevi chakari kwenye filamu ya Hatya ila ndani yake kukawa na uzuri wa kumuokowa Raja mtoto mdogo wa mwenye miaka mitano ni mtoto wa kike aliecheza kwenye filamu hiyo kama mwanaume.
Govinda alimsadia Raja kuepuka kifo kutoka kwa adui mkubwa wa filamu hiyo Joseph Sebastian Kapur.

Raja mtoto mdogo alitaka kuuliwa baada ya kuona wazazi wake Neelam Kothar na Anupam Kheir wakiuliwa, Kapur aliamini akimuuwa Raja atakuwa amepoteza ushahidi.
Govinda pamoja na ubaya wake wa kunywa Pombe masaa 24 ila alikuwa mzuri eneo jengine alimuokoa mtoto Raja, ushaudi ukapatika na wauwaji wakakamatwa.
Kwa sasa Govinda hayumo kwenye tansia ya Sanaa, tunakosa vitu vingi kutoka kwake kuna eneo naliona kabisa limepwaya hawa kina Salman Khan kazi mapezi tu filamu zao hazisisimuwi haziuzunishi hazitishi wala hazikuotowi machozi.

Kwa sasa Raja (Sujitha) ameolewa na anawatoto wawili.

Maoni