MAYANGA AMWITA EMMANUEL MARTIN TAIFA STARS



Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amemwongeza Kiugo wa Young Africans, Emmanuel Martin kwenye kikosi chake kinachojindaa kucheza na Botswana Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Maoni