JE WAJUA YANAYOJIRI KWENYE FUKWE HASA COCO BEACH?

HATARI! HATARI.

Polisi inawashikilia vijana 33 kwa makosa ya kuwahadaa wasichana kimapenzi ieleweke hapa kosa sio kuhadaa ila ni KUWABAKA. Vijana hao almaarufu kwa jina la beach boys au dunga dunga wanapatikana katika fukwe mbali mbali hapa Dar es salaam.

ISHU NZIMA IKO HIVI.

Watu wanapokwenda beach let say family kule beach wasichana wengi wanapenda kuogelea na wengi wao hawajui hivyo hawa beach boys hu take advantage na kuwakodisha mipira ya magari zile tubes halafu kuingia nao majini kuwa assist (Kuwafundisha kuogelea)

Kinachofuata sasa beach boy hupeleka boya hadi deep sea (kina kirefu) wakifika huko kijana huomba apewe penzi huku akimtishia mdada ukigoma nakuacha unafia hapa hapa.Mdada akijafanya mbishi anapewa advertise kwanza anaachwa anakunywa maji lita moja akishaona mlango wa kuzimu basi mweyewe anamuita kijana na kumpa kwichkwich huku wakielea majini kwa raha zao.

Kwa staili hii wadada wengi sana wanaliwa, wengi wamepewa mimba kwa staili hii, wengi wameambukizwa ukimwi kwa staili hii hii.Vijana hawa beach boys ndio imekua staili yao, wadada wakifika tu beach wao hugombania kuwafundisha kuogelea kumbe lengo ni kwenda kula mambo haya bila jasho.

Binti akishabakwa huko majini akirudi nchi kavu hasemi kilichomkuta huishia kulia tu kimoyomoyo.Kiukweli unaweza usiamini ila hebu vuta Picha upo kwenye kina kirefu then binti unaambiwa chagua moja nikuache ufe au unipe penzi?! Lazima utatoa kwa maana hakuna namna!

Huwa ninapokua beach kila weekend mara nyingi sio kuogelea ni kupunga upepo na kunywa  huwa naonaga sana mipira ikiwa inaelea deep sea katikati ya maji huku kukiwa na mwanamke na mwanaume lakini mawazo yangu yote najua ni mtu na mpenzi wake wanakula raha za dunia kumbe ni hawa vijana wahuni wanakula mambo bila jasho.

Nimepitia hii mada huko mtandaoni michango ya wachangiaji ni mingi sana, vijana wanakiri kwamba haya mambo yapo tena hata wake za watu wanaliwa saana tu.Unakuta family inafika ufukweni baba anakabidhi mkewe ufukweni  kwa vijana afundishwe kuogelea huku yeye akibaki ufukweni kashika kamera yake anachekelea tu na kukuna kitambi  kumbe hajui kule majini mkewe anapewa show amazing kana kwamba ndio Ada ya mafunzo.

Inasemekana kuna wengine hunogewa hasa ikiwa Show anayopewa ni ya kibabe kuliko anayoipata kwa mumewe ikifikia hapo mke kila week ataomba mumewe ampeleke beach kumbe anachokifuata ni#ShowYaKibabe

Kuna kijana anasema tena unakuta mke akipewa show hapa basi hatua 15 hivi binti yake nae anapewa show na kijana mwingine huku dingi katuliza kitambi chake ufukweni.

Kuna kijana amekiri jirani yao house girl alipewa show hadi kufika ufukweni akawa hawezi kutembea ukizingatia alikua muda mrefu hajapata mambo, sasa akiulizwa umepatwa na nini hasemi.

Kiufupi hali halisi ndio hii na maswali kujiuliza dada zangu hivi unakubali vipi mtu humjui akufudishe kuogelea?! Imagine mdada 'umenona' uko na chupi tu na sidiria upo ndani ya tairi dogo na mkaka kiasi kwamba uko zero distance mko katikati ya maji boya likiyumba kidogo unawahi kumkumbatia usianguke hivi huyu kijana hatakutamani kweli?  Unadhani hana matamanio?

Au unafikiri huyu kijana ni MALAIKA asipatwe na tamaa ya kimwili?Nawapa pole wadada wote ambao yamewakuta haya najua hata humu fb,whatsapp na instagram wapo ila hamuwezi kusema na kuficha kwenu kumepelekea jambo hili kutojulikana mapema na mabinti wengine wengi wakawa yanawafika hadi polisi walipojua na kuanza kuchukua hatua.

Maoni